Mshambuliaji wa
Yanga, Donald Ngoma ameonyesha ni mtu makini asiyetaka mchezo na kazi yake.
Ngoma alionyesha
hilo baada ya kuamua kubaki akifanya mazoezi binafsi baada ya yale ya pamoja
kama timu kumalizika.
Ngoma alikuwa
akipiga mikwaju ya penalti pekee yake mara tu baada ya Yanga kumaliza mazoezi
kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.
Mzimababwe huyo
alisema alikuwa akifanya hivyo ili kujiweka vizuri katika kazi hiyo kwa kuwa
amekuwa akikosa penalty mara kadhaa.
“Nataka kuhakikisha naifanya kazi ya kupiga penalty kwa uhakika, ndiyo maana nimeamua kufanya mazoezi,” alisema Ngoma ambaye tayari ameanza kuzivutia timu kubwa.
Hakuna maoni :