Mshitakiwa
namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na
washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.
Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.
Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari.
Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.
Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo.
Na Dotto Mwaibale
KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu
Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali
baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo
Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa
mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa
kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.
Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu
Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya
(51)
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter
Vitalis ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao
wanatuhumiwa kwa makosa mawili.
Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya
Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya
uhujumu uchumi.
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na
Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es
Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh.
bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya
Azam, baada ya kodi zote kutolewa.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na
Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza
majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata
hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza
kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo
hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo,
kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika
mahakama hiyo.
“Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana,” alisema Hakimu Shahidi
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani
hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto
mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine
ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama
upelelezi utakuwa umekamilika.
Hakuna maoni :