SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / TP MAZEMBE IKIWA NA SAMATTA, ULIMWENGU YANG'OLEWA KOMBE LA DUNIA KIPIGO CHA MABAO 3-0






TP Mazembe imeanza na mguu mbaya michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutolewa katika mechi ya kwanza tu kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kea Wajapan.

Sanfrecce Hiroshima ndiyo iliyotoa kipigo hicho kwa TP Mazembe ya DR Congo ambayo safu yake ya ushambuliaji inaongozwa na Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Kipigo hicho kinafuta ndoto za Watanzania hao kufika nusu fainali ya michuano hiyo na kukipiga na River Plate ya Argentina.

Wajapani walianza kupata bao lao la kwanza katika dakika ya 44 kupitia Yusuke Chajima likadumu hadi mapumziko.

Sanfrecce walipata bao la pili katika dakika ya 56 lililofungwa na Kazuhiko Chiba akifunga baada ya kuunganisha kona ya Chajima aliyepiga kona iliyozaa bao la kwanza.

Wakati Mazembe wakionekana kupambana kubadilisha mambo hasa baada ya Ulimwengu kuingia katika dakika ya 46, Sanfrecce  walifunga bao la tatu katika dakika ya 78 kupitia Asano aliyeunganisha krosi Mikic.

Adama Traore na Assale, nusura wafunge kutokana na kujaribu vizuri lakini mwisho mambo hayakuwa mazuri kwa Mazembe.

Sasa Sanfrecce Hiroshima inarudi dimbani Desemba 16 kuwavaa mabingwa wa Amerika Kusini River Plate wanaotokea Argentina.

Nusu fainali nyingine itakuwa siku inayofuata wakati mabingwa wa Ulaya, Barcelona watakapowavaa Guangzhou, kikosi kinachonolewa na Philipe Scolari.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply