SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / YANGA SC YATAMBA KUBEBA POINTI ZOTE SITA MKWAKWANI



YANGA SC ipo mjini Tanga tangu jana kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mgambo JKT na wamesema dhamira ni ushindi tu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro  amesema kwamba kikosi kipo imara na tayari kabisa kwa mchezo wa Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani.

“Tuko vizuri na tayari kabisa kuchukua pointi sita katika mechi zetu mbili mfululizo za Tanga,”amesema Muro na kuongeza; “Tunatambua itakuwa michezo migumu, lakini tumejipanga vizuri kwa ajili ya kushinda,”amesema.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga SC

Yanga itacheza na African Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, kabla ya kurudi tena kwenye Uwanja huo Jumatano kumenyana na ndugu zao, African Sports.

Ikumbukwe Ligi Kuu ilisimama kwa takriban mwezi mzima kupisha mechi za timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria mwezi uliopita na baadaye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.

Na wakati Ligi Kuu inasimama, Yanga SC ambao ndiyo mabingwa watetezi walikuwa katika nafasi ya pili kwa pointi zao 23, nyuma ya Azam FC iliyokuwa na pointi 25.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply