SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / C1C: NUSU FAINALI JUMANNE STOKE-LIVERPOOL, JUMATANO EVERTON-CITY.


C1C: NUSU FAINALI:
**Mechi zote Saa 5 Usiku, Saa za Bongo
Jumanne Januari 5
-Stoke City v Liverpool [Britannia Stadium]
Jumatano Januari 6
-Everton v Man City [Goodison Park]
+++++++++++++++++++++++
CAPITALONECUP-15Mechi za kwanza za Nusu Fainali ya C1C, Capital One Cup, ambalo ni Kombe la Ligi huko England, zitachezwa Jumanne Usiku Januari 5 na nyingine Jumatano Januari 6.

Jumanne Usiku, Stoke City wako kwao Britannia Stadium kuwakaribisha Liverpool na Jumatano ni huko Goodison Park kati ya Wenyeji Everton na Man City.

Nusu Fainali za C1C huchezwa kwa mikondo miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Timu hizi zitarudiana tena hapo Januari 26 na 27.

Timu hizi zilitinga Nusu Fainali kwa Stoke kuibwaga Sheffield Wednesday na Liverpool kuitoa Southampton wakati Everton waliwatoa Middlesbrough na Man City kuitupa nje Hull City.

Bingwa Mtetezi wa Kombe hili alikuwa Chelsea ambae alitupwa nje na Stoke City kwa Mikwaju ya Penati 5-4 baada ya Sare ya 1-1.

C1C: NUSU FAINALI:
Marudiano
**Mechi zote Saa 5 Usiku, Saa za Bongo
Januari 26
-Liverpool v Stoke City [Anfield]
Januari 27
-Man City v Everton [Etihad]

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply