Makubwa yamezidi kugundulika kwenye sakata la upotevu wa makontena
Bandari ya Dar na sasa inadaiwa kuwa kuna nyakati wahusika wamewahi
kufuta kumbukumbu za meli nzima ya makontena na kuiba makontena yote.
Taarifa hizo zinavuja wakati kukiwa na mvutano kati ya chama cha
Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kinachodai kutohusika kwa namna
yoyote na upotevu wa makontena zaidi ya 11,000 ambayo hayakulipiwa
ushuru bandarini (Wharfage charges).
TAFFA wanaitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuwajibika katika
upotevu huo ulioinyima Serikali kupitia mamlaka hiyo mabilioni ya fedha.
Chanzo: Raia Tanzania
Home
/
MATUKIO
/
Hali si Shwari Bandarini..Si Wizi Bali Kufuru..Meli Nzima Yaibwa, Wanjanja Waficha Nyaraka Kuonyesha Haikuwahi Kufika Tanzania
Hali si Shwari Bandarini..Si Wizi Bali Kufuru..Meli Nzima Yaibwa, Wanjanja Waficha Nyaraka Kuonyesha Haikuwahi Kufika Tanzania
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :