KIIZA AKISHANGILIA NA AJIBU... |
Hamisi
Kiiza ameshaifungia Simba mabao 12 msimu huu lakini ameweka wazi kuwa
hivi sasa shauku yake ni kuhakikisha timu yake hiyo inatwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara msimu huu.
Kiiza
alisema katika mzunguko huu wa pili uliobakia, wanahitaji kujituma kwa
nguvu zote ili kuweza kuisaidia timu hiyo kumaliza ligi katika nafasi
nzuri na hata ikiwezekana kutwaa ubingwa.
“Mechi
14 zilizobakia kwenye ligi ni nyingi, hivyo tunahitaji kujituma
ipasavyo kuweza kufanikiwa kushinda katika kila mechi, kuhakikisha
tunafanikiwa kutwaa ubingwa kwani lengo langu ni kuona tunafikia
malengo.
“Nipo
Simba kwa ajili ya kuisaidia na sihitaji maneno mengi zaidi ya kujituma
uwanjani na nitakuwa na furaha nikiona inafanikiwa kutwaa kombe,”
alisema Kiiza.
Hakuna maoni :