SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / LA LIGA: BARCA YAIBWAGA MTU 9 ATLETI.


BARCA-ATLETI-RC-FILIPELUISBarcelona wamepaa kileleni mwa La Liga baada ya kuwachapa Mtu 9 Atletico Madrid 2-1 katika Mechi iliyochezwa Nou Camp hii Leo.

Atletico walitangulia kufunga katika Dakika ya 10 kwa Bao la Koke na Barca kusawazisha Dakika ya 30 kupitia Lionel Messi na Dakika 8 baadae Luis Suarez akaipa Barca Bao la Pili na la ushindi.

Atletico walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 44 Filipe Luis kupewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya Messi.

Dakika ya 65 Diego Godin alipewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na kuiacha Timu yake Atletico ikiwa Mtu 9 na Bao 2-1 nyuma.

Bao hizo zilidumu hadi mwisho wa Mechi na kuifanya Barca izidi kuongoza La Liga ikiwa na Pointi 51 kwa Mechi 21 ikifuatiwa na Atletico wenye Pointi 48 kwa Mechi 22 na wa 3 ni Real Madrid wenye Pointi 44 kwa Mechi 21.

VIKOSI:
Barcelona: Bravo, Alves, Pique, Mascherano, Alba, Sergio, Rakitic, Iniesta, Suarez, Messi, Neymar
Akiba: Ter Stegen, Munir, Arda Turan, Sergi Roberto, Aleix Vidal, Vermaelen, Mathieu
Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Gimenez, Godin, Filipe, Augusto, Gabi, Saul, Koke, Carrasco, Griezmann
Akiba: Moya, Savic, Jesus Gamez, Oliver, Thomas, Jackson Martinez, Vietto.
REFA: Alberto Undiano
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Januari 30
FC Barcelona 2 Atletico de Madrid 1
2015 Getafe CF v Athletic de Bilbao
2015 SD Eibar v Malaga CF
2230 Villarreal CF v Granada CF
Jumapili Januari 31
0005 Real Sociedad v Real Betis
1400 Sevilla FC v Levante
1800 Valencia C.F v Sporting Gijon
2015 Las Palmas v Celta de Vigo
2230 Real Madrid CF v RCD Espanyol
Jumatatu Desemba 1
2230 Deportivo La Coruna v Rayo Vallecano

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply