Kocha Ahmed Morocco ameamua kuachana na ile ishu ya Ukurugenzi Mkuu wa Simba na kurudi zake kwao Zanzibar.
Hivi
karibuni, Morocco alipewa jukumu la kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars,
akisaidiana na Boniface Mkwasa kama kocha mkuu kabla ya Simba kumfuata
na kumpa kibarua cha kukinoa kikosi hicho.
Hiyo
ni siku chache tangu ifahamike kuwa kocha huyo wa Mafunzo ya Zanzibar,
huenda akasaini mkataba wa miezi sita wa kuwa mkurugenzi mkuu chini ya
Mganda, Jackson Mayanja.
Morocco
alisema kila kitu kilikwenda vizuri kuhusiana na kusaini mkataba
kuanzia akiwa Unguja, Zanzibar, hadi alipofika jijini Dar es Salaam,
lakini ghafla anashangaa rais wa Simba kubadilika.
“Hapa
ninapoongea tayari nina nakala kutoka TFF inayoniruhusu kuifundisha
Simba, nilikuwa nipo tayari kufanya nao kazi hata leo (jana), lakini
makubaliano ya kimkataba tuliyokubaliana yamekuwa kinyume.
“Makubaliano
tuliyokubaliana na Simba pamoja na TFF ni kuitumikia timu hiyo kwa
kipindi cha miezi minne na kama ingetokea nimepata majukumu ya kwenda
kuitumikia timu ya taifa, basi ningefanya hivyo.
“Lakini
cha ajabu na kushangaza leo (jana) asubuhi, rais wa Simba ghafla
alibadilika katika hatua za mwisho kitu ambacho sijakitegemea kabisa,
katika suala la mshahara ambao tulikuwa tumekubaliana tangu nilipokuwa
Zanzibar limebadilishwa kwa kiwango kikubwa, sasa mimi nimeondoka nipo
zangu Zanzibar, kama litatokeo lolote jipya nitarudi,”alisema Moroco.
Hakuna maoni :