Mshambuliaji
Mbwana Samatta, juzi Jumatano amerejea katika klabu yake ya TP Mazembe
ya DR Congo, amejikuta katika mazingira mapya baada ya kukabidhiwa kwa
kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Togo, Hubert Velud.
Velud
raia wa Ufaransa ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa Paris FC mwaka 1995
mpaka 1999, ambayo kwa sasa inashiriki inashiriki Ligue 2 ya Ufaransa,
ametua Mazembe akitokea Klabu ya USM Alger ya Algeria na kuchukua mikoba
ya Mfaransa mwenzake Patrice Carteron.
Samatta
ambaye alikuwa mbioni kutua Genk ya Ubelgiji, dili lake lilikwama
kutokana na mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi kugoma kumuachia.
Meneja
wa Samatta, Jamal Kisongo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa nyota huyo
amerejea katika kituo chake cha kazi ili kuweza kuongeza msukumo wa
kuondoka kutokana na Katumbi kutokuwa tayari kupata hasara kutoka kwa
straika huyo.
“Samatta
tayari amerejea Congo…Hili litasaidia kumpa presha Katumbi ya kumuuza
maana hatoweza kukubali apate hasara ya jumla, hivyo atalazimika
kukubali matakwa ya mchezaji mwenyewe.
“Lakini
pia tumeacha nafasi kwa serikali nayo ione inaweza kutusaidia vipi kwa
kuwasiliana na Katumbi ili kuweza kulimaliza jambo hili,” alisema
Kisongo.
Hakuna maoni :