SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Unlabelled / SAMTTA KUPITA MITAA YA DAR KUWAONYESHA WATANZANIA TUZO YAKE, JUMUIKA NAYE TAFADHARI



Mwanasoka Bora Afrika Mbwana Samatta, leo atapiga na tuzo yake aliyotwaa jijini Lagos, Nigeria juzi. Tuzo hiyo ataipitisha katika baadhi ya mitaa ya Dar es Salaam wakati akienda Escape One ambako atakutana na mashabiki watakaotaka kujumuika naye.

Salehjembe imeiona ratiba hiyo mtandaoni na kutaka kujua kama ni sahihi naye akasema:

"Ni kweli nitakutana na waziri leo, tutajumuika leo pale Kempinsky na baada ya hapo tutapita baadhi ya sehemu kwenda huko Escape One. Ila bado sijajua kuwa njia gani hasa tutakazopita," alisema

RATIBA ILIYOTOLEWA MTANDAONI AMBAYO HAIJAELEZA MTOAJI NI NANI, IKO HIVI:
Saa 10 Jioni atakua na press conference na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye Kempisky Hotel.

Baada ya hapo msafara kwenda Escape one utaanza kupitia mitaa ya Samora, clock tower, Mnazi mmoja, barabara ya Uhuru, Kamata, hadi karume.

Kisha barabara ya Kawawa kuanzia ofisi ya mkuu wa mkoa, kigogo, magomeni usalama, kinondoni, hadi morocco, na kuifuata barabara ya Ally Hassan mwinyi kupitia Victoria, Makumbusho, Sayansi, Bamaga hadi Mwenge.

Msafara huo utazungukia Kawe, Lugalo, mlalakuwa na kumalizikia Escape one ambapo wanamichezo na wasanii mbalimbalo watapata nafasi ya kupiga nae picha na kumpongeza.


Watu wote wanaombwa kujitokeza barabara sehemu ambazo msafara wa shujaa Mbwana Ally Samatta utapita.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply