Pamoja
ya viungo wa Simba, Mzimbabwe, Justice Majabvi na Jonas Mkude kuonekana
muhimili mkubwa wa kikosi cha Simba kwa sasa, kiungo wa kimataifa wa
Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amesema kwake anawaona ni wachezaji
wa kawaida tu.
Hiyo
imekuja ikiwa zimesalia siku tano pekee kabla ya mechi baina ya wababe
hao itakayopigwa Februari 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
ambapo fukuto la mchezo huo limeshaanza kuwagubika mashabiki wa timu
hizo mpaka wachezaji wenyewe.
Niyonzima
ambaye juzi Jumamosi alifanikiwa kuiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de
Joachim SC ya Mauritius, pia ameelezea jinsi anavyoelewana na kiungo
mwenzake, Mzimbabwe Thabani Kamusoko pale inapotokea wamepangwa pamoja,
hivyo anaamini watafanya kazi nzuri.
| MAJABVI |
“Naweza
kusema mechi ya Simba ni ngumu ila kwa upande wetu wachezaji
tunajiandaa vizuri kwa ajili ya kufanya kazi yetu vizuri na mwisho wa
siku tuibuke na ushindi katika hiyo mechi, Mkude na Majabvi naona ni wa
kawaida tu, nafikiri tusubiri tutaona siku ya mechi.
“Kombinesheni
yangu na Kamusoko ni nzuri kwa sababu tunajuana muda mrefu, kwa hiyo
inakuwa rahisi kuelewana tukiwa uwanjani,” alisema Niyonzima.
Siku
chache zilizopita, Mkude aliwahi kunukuliwa akiionya Yanga kuelekea
katika mchezo wao huo akiitahadharisha kuwa makini kutokana na uimara na
spidi waliyonayo kwa sasa katika kushinda mechi zao mfululizo za Ligi
Kuu Bara.


Hakuna maoni :