Mashabiki wa Bastia ya Ufaransa wamezua sekeseke ikiwa ni pamoja na kushambulia kituo cha Polisi cha mji wa Bastia,.
Licha ya timu yao kushinda, mashabiki hao walifanya vurugu na wenzao wakakamatwa na askari polisi.
Lakini mashabiki hao walionekana kupinga suala hilo na kutaka wenzao waachiwe kwa nguvu tena mara moja.
Walipoona
jambo hilo halitekelezwi, walipambana kwa kuvamia kituo cha polisi cha
Bastia na inaelezwa askari mmoja aliumizwa kichwani.
Vurugu
zilikuwa kubwa, huku mashabiki hao wakiunguza baadhi ya sehemu. Baadaye
walivunja vioo vya magari pamoja na kuyaunguza mengine.
Baadaye polisi walivamia eneo hilo na kuwakamata baadhi waliokuwa wamefunika nyuso zao.









Hakuna maoni :