SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / TFF-YAIPA ‘5’ AFRICAN LYON KUPANDA LIGI KUU VODACOM, YASIKITIKA MWANDISHI ‘KUPIGWA’ NA MWINYI KAZIMOTO WA SIMBA.


TFF-LEO-TOKA-TFFShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeipongeza timu ya African Lyon FC ya jijini Dar es salaam kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao, baada ya kuwa vinara wa Kundi A katika ligi hiyo iliyomalizika jana. 

African Lyon imeungana na timu ya Ruvu Shooting FC ya Mlandizi mkoa wa Pwani iliyokua timu ya kwanza kupanda ligi kuu wiki iliyopita kutoka kundi B.

TFF inaitakia kila la kheri Africa Lyon FC katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom, kwa kujiandaa vizuri na mikiki mikiki ya VPL ambayo ina jumla ya timu 16 na kila klabu kucheza jumla ya michezo 30 kwa msimu nyumbani na ugenini.


TFF YASIKITISHWA KUPIGWA KWA MWANDISHI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kupigwa kwa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Mwanaspoti nchini, Mwanahiba Richard na kiungo wa timu ya Simba SC Mwiny Kazimoto mjini Shinyanga. 

Kufuatia kitendo hicho kilichotokea wakati wa mazoezi, TFF imesema tukio liliofanywa na mchezaji huyo ni kinyume na sheria, taratibu/kanuni zinazoendesha mpira wa miguu nchini, hivyo wanakilaani kitendo hicho kwa nguvu zote.

Kwa kuwa tukio lilitokea wakati wa mazoezi, mpaka sasa TFF bado haijapokea taarifa rasmi kuhusiana na suala hilo.
IMETOLEWA NA TFF

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply