Mbeya
City imeionyesha Toto African namna ya kutembea katika jiji la Mbeya
baada ya kuichapa kwa mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Ramadhani
Chombo 'Redondo' aliifungia Mbeya City mabao mawili, vivyo hivyo Haruna
Moshi 'Boban' naye akafunga mawili pia kabla ya Meshack Samwel kufunga
la tano.
Mbeya City imeibuka na ushindi huo wa kishindo ikiwa inacheza kwa mara ya kwanza chini ya Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri.
Mjini
Tanga, African Sports wameamka baada ya kuichapa Mgambo Shooting kwa
bao 1-0. Na Kagera Sugar ikagawana pointi na JKT Ruvu kwa sare ya bao
1-1.

Hakuna maoni :