VPL-LIGI KUU VODACOM
Matokeo:
Jumamosi Februari 13
Stand United 1 Simba 2
Mgambo JKT 0 African Sports 1
Mbeya City 5 Toto Africans 1
Ndanda FC 1 Majimaji 0
JKT Ruvu 1 Kagera Sugar 1
BAO
2 za Straika kutoka Uganda, Hamisi Kiiza, Leo zimewapa ushindi wa Bao
2-1 Simba walipocheza na Stand United huko Kambarage Jijini Shinyanga na
kuwapa uongozi wa Ligi Kuu Vodacom, VPL.Simba sasa wapo kileleni wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi 19 wakiguatiwa na Yanga wenye Pointi 43 kwa Mechi 18 na wa 3 ni Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 16.
Hadi Mapumziko, Simba walikuwa mbele 1-0 na Kipiundi cha Pili Kiiza tena kuwapa Bao la pili na mwishoni Stand United kufunga Bao lao moja.
Huko Sokine, Mbeya, Wenyeji Mbeya City waliitwanga Toto Africans Bao 5-1 kwa Bao za Rafael, Ramadhan Chombo, Boban, Bao 2 na Meshak.
Mechi inayofuata kwa Simba kwenye VPL ni Jumamosi ijayo ambapo wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza Dabi ya Kariakoo na Watani zao Yanga ambao Wikiendi hii hawana Mechi ya VPL kwa vile Leo walikuwa huko Visiwani Mauritius kucheza Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI walipoipiga Cercle de Joachim 1-0 kwa Bao la Donald Ngoma.
VPL-LIGI KUU VODACOM
Ratiba
Jumapili Februari 14
Mwadui FC v Tanzania Prisons
Coastal Union v Azam FC
Jumamosi Februari 20
Yanga v Simba
Mgambo JKT v Tanzania Prisons
Stand United v JKT Ruvu
Mbeya City v Azam FC
Majimaji v Mtibwa Sugar
Toto Africans v Kagera Sugar
Jumapili Februari 21
Ndanda FC v African Sports
Mwadui FC v Coastal Union

Hakuna maoni :