SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / EMIRATES FA CUP:CHELSEA YAITWANGA MAN CITY 5-1 YATINGA ROBO FAINALI.


FA CUP
Matokeo:
Raundi ya 5
Jumapili Februari 21
Blackburn 1 West Ham 5   
Tottenham 0 Crystal Palace 1      
Chelsea 5 Man City 1
++++++++++++++++++
EMIRATES-FACUPWest Ham, Crystal Palace na Chelsea Leo zimeweza kutinga Robo Fainali ya EMIRATES FA CUP kwa kishindo baada ya kupata ushindi mnono.

West Ham na Crystal Palace zote zilishinda Ugenini kwa West Ham kuishindilia Blackburn Rovers Bao 5-1 na Crystal Palace kuitungua Tottenham 1-0.

Katika Mechi ya mwisho hii Leo, Chelsea, ikicheza kwao Stamford Bridge, iliibamiza Man City, iliyochezesha Kikosi dhaifu, Bao 5-1.
Bao za Chelsea zilifungwa na Diego Costa, Dakika ya 35, Willian, 48, Gary Cahill, 53, Eden Hazard, 67, na Traore, 89, wakati lile la City lilifungwa Dakika ya 37 na David Faupala.

VIKOSI:
Chelsea (Mfumo 4-2-3-1): Courtois; Azpilicueta, Cahill, Ivanovic, Baba Rahman; Fabregas, Mikel; Pedro, Willian, Hazard; Diego Costa.
Akiba: Begovic, Miazga, Matic, Loftus-Cheek, Oscar, Traore, Remy.

Manchester City (Mfumo 4-4-2): Caballero; Zabaleta, Adarabioyo, Demichelis, Kolarov; M Garcia, Fernando, A.Garcia, Celina; Iheanacho, Faupala.
Akiba: Hart, Clichy, Humphreys, Kompany, Fernandinho, Barker, Sterling.

REFA: Andre Marriner

EMIRATES FA CUP

Raundi ya 5
Jumatatu Februari 22
2245 Shrewsbury v Man United

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply