Mkurugenzi
mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu
Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia
mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati
akizungumza na simu.
Kamanda
wa polisi wa MKOA wa Tanga Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo
ilitokea juzi SAA 2;30 usiku katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya
himo mjini Korogwe.
Alisema
Mberesero ambae mabasi yake hufanya safari Kati ya mikoa ya
Arusha,tanga,Daresalaam na singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya
kituo cha mafuta cha Lake oil na kugongwa na gari hilo.
Mfanyakazi
wa kampuni hiyo ,Adam Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe
kuangalia Kiwanja kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta.
Kama
unavyojua bosi wetu pamoja na kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa
anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam
na Arusha,hivyo alipokuja Tanga alituambia anakwenda Korogwe kuangalia
Kiwanja cha kujenga kituo kipya cha mafuta,alisema Adam.
Alisema
bosi wake huyo alikuwa ameliweka gari lake katika kituo cha mafuta cha
Lake oil na kwamba alishuka kwajili yakuelekea katika Kiwanja hicho.
Wengi waliokuwepo eneo la ajali hawakujua kama ni yeye hadi tulipokwenda kuchukua mwili wake ndipo wakashtuka,Alisema.
Kamanda Mihayo alisema wanamsaka Dereva aliyesababisha ajali hiyo kwa uzembe na kusababisha kifo.
Home
/
MATUKIO
/
TANZIA: Mmiliki wa Mabasi ya Ngorika, Stephen Mberesero Afariki Dunia..Agongwa na Gari Akiongea na Simu Segerea.
TANZIA: Mmiliki wa Mabasi ya Ngorika, Stephen Mberesero Afariki Dunia..Agongwa na Gari Akiongea na Simu Segerea.
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :