| YONDANI |
Kikao
cha Kamati ya Kusimamia na Kuendesha ligi (Kamati ya Masaa 72)
kimekutana Jumatano katikati ya wiki kupitia taarifa na ripoti
mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu (VPL), na Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
zinazoendeea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali nchini.
Ligi Kuu ya Vodacom
Mchezaji
Kelvin Yondani wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh
500,000 (laki tano) baada ya kumpiga usoni kwa box la dawa Dk Mganga
Kitambi wa Coastal Union wakati akitoa huduma kwa kipa wake katika mechi
namba 121 kati ya timu hizo iliyofanyika Januari 30, 2016 kwenye Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga.
Yondani
alitenda kosa hilo baada ya kumuomba maji Daktari huyo, lakini
akamnyima. Adhabu huyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi
Kuu Toleo la 2015 ambapo baada ya kutumia adhabu ya mechi hizo,
hataruhusiwa kucheza hadi atakapokuwa amelipa faini hiyo.
Naye
Dk Kitambi anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kitendo chake cha
kumrudishia Yondani kwa kumpiga ngumi. Kitendo cha Daktari huyo ni
kinyume cha Kanuni ya 41(2), na pia Kanuni ya 36 kuhusu mchezo wa
kiungwana.
Klabu
ya Yanga imepigwa faini ya Sh 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni
ya 42(1) kutokana na washabiki wake kuwatupia chupa za maji wachezaji wa
Coastal Union walipokuwa wakishangilia bao la pili.

Hakuna maoni :