SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / BARCA V ARSENAL: LEO NDANI YA MDOMO WA SIMBA NOU CAMP, WENGER AJITETEA.

BARCA-ARSENAL-WENGERvMSNMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger, ambayo Timu yake Leo iko huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kurudiana na Miamba ya Soka Duniani FC Barcelona katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI huku wakiwa wamepigwa 2-0 katika Mechi ya kwanza, amejitokeza na kutetea rekodi yake Klabuni.

Kufuatia kufungwa 2-1 na Watford Jumapili iliyopita Uwanjani Emirates na kutupwa nje ya FA CUP, Kombe ambalo walilibeba kwa Misimu Miwili iliyopita, Mashabiki wa Arsenal walimtaka Wenger afungashe virago vyake na kutimka.

Hali hiyo pia imekuja baada ya Arsenal kujikuta wako Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City wakati walikuwa wakienda vizuri tu mwanzoni mwa Msimu.

Akiongea na Wanahabari huko Barcelona kuhusu Mechi yao ya Leo, Wenger alibaki kuitetea rekodi yake Klabuni Arsenal tangu ajiunge nao Mwaka 1996.

Alisema: “Nimeijenga Klabu kwa kufanya kazi kwa bidii, bila msaada wowote toka nje, na ukichukulia wapi tulipo Leo na tulipokuwa nilipoingia, utaona tumesonga mbele na tena bila ya pesa toka kwa Mtu yeyote bali kwa pesa za jasho letu!”

Aliongeza: “Tatizo ukikaa sehemu muda mrefu Watu wanahoji utumishi na uwezo wako lakini mie sina wasiwasi na natumia muda wangu mwingi kwa Klabu na nina motisha kubwa!”

Alipoulizwa kama anakerwa kupondwa na Mashabiki, Wenger alijibu: “Sitaki kuingia kwenye mjadala huo kwani unaweza kutafsiriwa kwa namna mbili.”

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply