SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MASHABIKI WA KIGALI WANA HAMU KUPITILIZA KUONA MAMBO YA KAMUSOKO.


Kiungo Thabani Kamusoko ni kati ya wale mashabiki wanatamani kesho ifike ili waione kazi yao wakati Yanga itakapoivaa APR katika mechi ya Ligi ya Mabingwa mjini Kigali, Rwanda.

Mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, lakini mashabiki wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na kiungo huyo Mzimbabwe.

Gumzo la Kamusoko ni baada ya mashabiki wa Rwanda kupata taarifa kwamba pamoja na kuondoka kwa Niyonzima wakati alipokuwa na mgogoro na klabu ya Yanga, Kamusoko alionekana ndiye angekuwa jibu.
Mashabiki hao waliojitokeza kwenye mazoezi ya Yanga tokea jana, leo pia walikuwa wakimfuatilia kwa karibu.

Wengi wanaonyesha wana hamu ya kumuona akicheza, pia hasa baada ya kusikia Niyonzima ambaye wanaamini ni kiungo bora kabisa analazimika kucheza namba 11 na kumuachia Kamusoko acheza namba 8 ambayo Niyonzima amekuwa akiishikilia anapokuwa na kikosi cha Rwanda ‘Amavubi’ au alipokuwa APR.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply