Mbeya City imepata ushindi wake wa sita katika Ligi Kuu Bara baada ya kuishinda Stand United kwa mabao 2-0.
Katika
mechi hiyo kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wenyeji Mbeya City
walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao moja lililofungwa na
Raphael Alfa.
Kipindi
cha pili waliongeza bao jingine kupitia beki wake Ramadhani Shamte na
kuwapunguza kasi Stand United waliokuwa wakipambana kusawazisha.
Kwa ushindi huo, Mbeya City sasa wamefikisha pointi 24 na kupanda hadi nafasi ya nane wakitoka nafasi ya 10.
Hakuna maoni :