DHAIRA WAKATI AKIWA SIMBA |
Uongozi
wa Simba umeahidi kushirikiana na familia ya kipa wake wa zamani, Abel
Dhaira ambaye amegundulika kuugua kansa ya utumbo.
Msemaji
wa Simba, Haji Manara amesema: "Dhaira ni kati ya wachezaji waliopita
Simba. Kilichomkuta ni kitu kigumu na tunaungana naye katika kipindi
hiki.
"Tutashirikiana
naye pamoja na familia yake katika kipindi hiki ili kuonyesha upendo wa
umoja wakati wa furaha, pia wakati wa matatizo," alisema Manara.
Dhaira,
mtoto wa kipa nyota wa zamani wa Uganda Bright Dhaira alikuwa anakipiga
katika kikosi cha BV Vestmannaeyjar cha Iceland hadi alipoanza kuugua.
Baada ya kuzidiwa, alikuwa amerejea nyumbani kwao Uganda katika mji wa Jinja kuwatembelea ndugu na familia yake.
Alikimbizwa katika hospitali jijini Kampala na inaelezwa bado hali yake si ya kuridhisha.
Simba
inakuwa klabu ya pili kuungana na Dhaira katika wakati huo mgumu baada
ya BV Vestmannaeyjar kutangaza itapitisha harambee kumchangia ili apate
fedha kupunguza gharama za matibabu.
Hakuna maoni :