SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / SIMBA YAUNGANA NA DHAIRA, YASEMA ITASHIRIKIANA NA FAMILIA YAKE BEGA KWA BEGA.

DHAIRA WAKATI AKIWA SIMBA

Uongozi wa Simba umeahidi kushirikiana na familia ya kipa wake wa zamani, Abel Dhaira ambaye amegundulika kuugua kansa ya utumbo.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema: "Dhaira ni kati ya wachezaji waliopita Simba. Kilichomkuta ni kitu kigumu na tunaungana naye katika kipindi hiki.

"Tutashirikiana naye pamoja na familia yake katika kipindi hiki ili kuonyesha upendo wa umoja wakati wa furaha, pia wakati wa matatizo," alisema Manara.

Dhaira, mtoto wa kipa nyota wa zamani wa Uganda Bright Dhaira alikuwa anakipiga katika kikosi cha BV Vestmannaeyjar cha Iceland hadi alipoanza kuugua.

Baada ya kuzidiwa, alikuwa amerejea nyumbani kwao Uganda katika mji wa Jinja kuwatembelea ndugu na familia yake.

Alikimbizwa katika hospitali jijini Kampala na inaelezwa bado hali yake si ya kuridhisha.

Simba inakuwa klabu ya pili kuungana na Dhaira katika wakati huo mgumu baada ya BV Vestmannaeyjar kutangaza itapitisha harambee kumchangia ili apate fedha kupunguza gharama za matibabu.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply