Uongozi wa Simba umesema utaendelea kutoa “full support” kwa Kocha Mkuu, Jackson Mayanga raia wa Uganda.
Uamuzi
huo unatokana na namna kocha huyo alivyoonyesha juhudi kubwa katika
kukibadilisha kikosi chake hata kuliko makocha waliopita, wakiwemo
waliotokea barani Ulaya.
Makamu
wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema uongozi utafanya
hivyo ili kuhakikisha kikosi chao kinaendelea kupambana.
“Tunaona mchango wa wachezaji, tunaona mchango mkubwa wa kocha. Hakika lazima tuwaunge mkono kwa nguvu kabisa.
“Tuko pamoja na kocha kwa kuwa tunaona juhudi zake na uongozi umemuahidi kuendelea kumuunga mkono na itakuwa hivyo.
“Pia
tuko pamoja na wachezaji na lengo letu ni kuona vijana wanapambana hadi
mwisho. Hali ya timu inaimarika kila siku, jambo linalotupa moyo
kuendeleza ushirikiano huo,” alisema Kaburu.
Mayanja
aliingia Simba kama kocha msaidizi chini ya Dylan Kerr raia wa
Uingereza ambaye alitimuliwa hata kabla ya Mayanga kuanza kazi.
Baada
ya hapo, Simba ilisitisha kutafuta kocha mkuu baada ya kuona Mayanja
alikuwa akifanya vziuri katika mechi zake zote za mwanzo, tena
mfulilizo.
Hakuna maoni :