AJIB (KULIA... |
Wekundu
wa Msimbazi yaani Simba, kesho wanacheza na Toto Africans katika Ligi
Kuu Bara lakini straika wake, Ibrahim Ajib amesema kamwe Yanga haiwezi
kuwazuia kutwaa ubingwa msimu huu.
Kauli
hiyo ya Ajib imekuja Simba ikiwa kileleni mwa ligi hiyo na pointi 57
huku Yanga ikifuatia na pointi 56 na Azam FC ni ya tatu ikiwa na pointi
55.
Ajib
ambaye ana mabao tisa katika ligi kuu, alisema kwa upande wao hawezi
kuihofia kasi ya Yanga kwani haiwezi kuwazuia kutimiza lengo lao la
kutwaa ubingwa.
“Unajua
hatuna cha kuhofia kwa sasa zaidi ya kuipigania nafasi hii iliyobaki
ili tuweze kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, kushinda kwa
Yanga michezo yake ya viporo isiwe sababu ya sisi kukata tamaa.
“Jambo
la msingi kwetu ni kujipanga na kupambana kwani Yanga kitu gani mpaka
tushindwe kuchukua ubingwa? Naamini wachezaji na viongozi wote malengo
yetu ni kutwaa ubingwa, hilo lipo wazi,” alisema Ajib.
SOURCE: CHAMPIONI
Hakuna maoni :