MCHEZAJI wa Newcastle United Papiss Cisse amepigwa Faini Mahakamani kwa Makosa ya Kuendesha Gari bila ya Leseni halali na kisha hapo hapo kutakiwa kila la heri kwenye vita ya Timu yake ya kuepuka kushushwa Daraja kutoka Ligi Kuu England.
Cisse, Mchezaji wa Kimataifa wa Senegal, alipatikana na hatia ya kutumia Leseni iliyomalizika muda wake na kupigwa Faini ya Pauni 547 na pia kukatwa Pointi 4 kwenye Leseni yake na Hakimu wa Mahakama ya Newcastle, Carolyn Hyslop, ambae pia alimwambia: “Kila la Heri Kesho!”
Leo Newcastle United wapo kwao St James' Park kucheza na Swansea City katika Mechi ya Ligi Kuu England ikiwa watataka wasiporomoshwe Daraja.
Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa Cisse alisimamishwa na Polisi Mjini Newcastle Februari 2015 walipomtaka ashushe Kioo cha mbele cha Gari yake kwa vile kilikuwa cheusi mno.
Hapo ndipo Polisi walipogundua Leseni yake ya Nje iliyopewa ridhaa ya kutumika Uingereza kwa Mwaka Mmoja imekwisha muda wake na kumtaka aibadili iwe ya Uingereza.
Lakini, Mwaka huo 2015, Mwezi Mei na Julai, Cisse tena alisimamishwa na Polisi na kukutwa na Leseni ile ile ya nje ambayo imekwisha muda wake wa kutumiwa Uingereza na kuburuzwa Mahakamani.
Hakuna maoni :