SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / LEO YANGA KURUDI SEHEMU YAKE, KUIMWAGA SIMBA KILELENI.


LIGI KUU VODACOM                             
Ratiba:
Jumamosi Aprili 16
Coastal Union v JKT Ruvu  
Yanga v Mtibwa Sugar
Ndanda FC v Kagera Sugar

VPL-SIT-LOGO-1MABINGWA wa VPL, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga, Leo wako Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakimalizia kiporo chao na kuwa na kazi moja tu ya kushinda na kuishusha VPL-APR13Simba toka kileleni.

Yanga Leo wanacheza na Mtibwa Sugar Timu ambayo iko Nafasi ya 4 na tayari unaweza kusema ishamaliza Ligi kwani haiwezi kutwaa Ubingwa, kuchukua Nafasi ya Pili au kushushwa Daraja na hivyo Mechi zilizobaki ni kukamilisha Ratiba tu.

Kwa Yanga, ushindi au hata Sare tu, itawang’oa Simba kileleni na wao kutwaa uongozi huku Mechi zikibaki 6 kwao.

Simba wanaongoza VPL wakiwa na Pointi 57 kwa Mechi 24 na Yanga ni wa 2 wakiwa na Pointi 56 kwa Mechi 23 huku Azam FC wakiwa ni wa 3 wakiwa na Pointi 56 kwa Mechi 24.

Mechi nyingine zitakazochezwa Leo ni zile za Ndanda FC wakiwakaribisha Kagera Sugar katika Uwanja wa Nang’wanda Sijaona Mjini Mtwara, Coastal Union wakiikaribisha JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO-Timu za juu:
VPL-TIMUZAJUU-APR15                             
Ratiba:
Jumapili Aprili 17
Simba SC v Toto Africans 
 
Jumatano Aprili 27
Azam FC v Majimaji
Yanga v Mgambo JKT 
      
Jumamosi Aprili 30
Toto Africans v Yanga       
Simba SC v Azam FC        
African Sports v Coastal Union    
Mwadui FC v Stand United
Mtibwa Sugar v Mbeya City

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply