Baada
ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Ligi
Kuu Bara, kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameamka na kusema,
anakubali kufungwa lakini akasisitiza, walicheza mechi kwenye uwanja
mbovu.
Toto
African ndiyo walioichapa Mwadui FC kwa bao 1-0, katika mechi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Dar es Salaam. Shujaa wa
Toto akiwa ni Waziri Junior aliyepachika bao hilo katika kipindi cha
kwanza.
“Nakubali kabisa kuwa mchezo nimepoteza kwa kuwa bao lilikuwa hakuna lawama hata kidogo. Tumepambana mwisho ukashindikana.
“Lakini uwanja tuliochezea, unaweza ni wa kuchezea ng’ombe na si binadamu. Hauna viwango na kweli umeharibika sana.
“Awali
tulikuwa tucheze Jumamosi, eti mechi ikaahirishwa kwa kuwa kuna Fiesta
na ajabu ligi ilishapangwa, kwa kuwa kuna shughuli ambayo si ya soka,
mechi inaahirishwa,” alisema Julio.
Katika
mechi hiyo, Mwadui FC walishindwa kung’ara katika kipindi cha kwanza,
lakini wakacharuka katika kipindi cha pili lakini hakukuwa na mafanikio.
Hakuna maoni :