YANGA
SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia
ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga jioni ya leo.
Bao hilo pekee la mabingwa hao watetezi lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe, Thabani Scara Kamusoko katika dakika ya 95 na kuwarejesha wana Jangwani hao kileleni.
Kamusoko
alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kichwa ya
Mzimbabwe mwenzake, Donald Dombo Ngoma ambaye naye alipokea krosi ya
winga Godfrey Mwashiuya.
Yanga SC
inafikisha pointi 26, baada ya kucheza mechi 11, ikiizidi pointi moja
Azam FC yenye mechi moja mkononi, ambayo sasa inachukia nafasi ya pili.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo
Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent
Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Malimi
Busungu, Donald Ngoma na Deus Kaseke/ Godfrey Mwashiuya.
African Sports; Ramadhani Mwaluko,
Mwaita Ngereza, Khalfan Twenye, Juma Shemvuni, Rahim Juma, Mussa
Chambega/Ally Ramadhani ‘Kagawa’,
Mussa Kizenga/James Mendi, Pera Ramadhani, Hassan Materema, Mohammed Mtindi/Hussein Issa na Mohamed Issa.
Hakuna maoni :