Simba
imeiangushia mvua ya mabao Kimbunga FC ya Zanzibar katika mechi ya kirafiki
mjini humo.
Simba
iliyotawala mchezo huo ikiwa ni sehemu ya kambi yake kujiandaa na Ligi Kuu
Bara, ilianza kupata bao la kwanza katika dakika ya 14 kupitia Ibrahim Ajibu,
ikaongeza la pili dakika ya 32 kupitia Danny Lyanga.
Nahodha
Mussa Hassan Mgosi akaongeza bao la tatu katika dakika ya 38 na Simba ikaenda
mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.
Kipindi
cha pili, Kimbunga walipata bao la pili, lakini Simba ikafunga mengine mawili
kupitia Ajibu.
Mchezo
ulikuwa mzuri lakini kocha wa Simba, Dylan Kerr alitoa zaidi ya wacheaji wanne
akionekana alitaka kukipima hasa kikosi chake.
KIKOSI:
Peter Manyika
Emery Nimubona
Said Issa
Nova Lufungo
Mohamed fhaki
Abdi Banda
Mwinyi Kazimoto
Mussa mgosi
Joseph Kimwaga
Ibrahim Ajibu
Danny Lyanga
WALIOTOKA:
Mgosi
Emery
Kimwaga
Kzimoto
WALIOINGIA:
Ugando
Mwalyanzi
Majwega
Saleh khamis
Hakuna maoni :