SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / ADEBAYOR AREJEA LONDON, ASAINI PALACE.


ADEBAYOR-PALACEBAADA ya kutokuwa na Timu tangu Mwaka Jana baada ya kuachwa na Timu yake Tottenham Hotspur, Straika wa Kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor, amerejea tena Jijini London Nchini England na kujiunga na Klabu ya Ligi Kuu England Crystal Palace.

Adebayor alifutiwa Mkataba na Tottenham Septemba Mwaka Jana baada ya Klabu hiyo kumlipa Fedha zake zote za kipindi chake chote kilichobaki kwenye Mkataba.

Crystal Palace imethibitisha kumsaini Straika huyo wa Miaka 31 kama Mchezaji Huru kwa Mkataba hadi mwishoni mwa Msimu huu.

Adebayor alitua kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu England alipojiunga na Arsenal kutoka Klabu ya France Monaco Mwaka 2006 na kisha mwanzoni mwa Msimu wa 2009/10 kujiunga na Manchester City kwa Dau la Pauni Milioni 25.

Kisha akaenda kwa Mkopo huko Real Madrid na Tottenham na Agosti 2012 kubadili Mkataba wake na Tottenham kuwa wa kudumu.

Crystal Palace-Dirisha la Uhamisho Januari 2016:
NJE
Jake Gray (Huddersfield Town) Mkopo
Jack Hunt (Sheffield Wednesday)

LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumanne 2 Februari 2016
[Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Southampton              
Leicester v Liverpool                  
Norwich v Tottenham                 
Sunderland v Man City               
West Ham v Aston Villa 
             
[Mechi kuanza Saa 5 Usiku]
Crystal Palace v Bournemouth               
Man United v Stoke          
West Brom v Swansea   
             
Jumatano 3 Februari 2016
[Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Everton v Newcastle         
Watford v Chelsea

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply