SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / PATO MKOPO CHELSEA, TOWNSEND ATUA NEWCASTLE, MAN UNITED, VAN GAAL WAREJEA MAZOEZINI.


PATO KUTUA CHELSEA MKOPO MIEZI 6!
MANUNITED-MASHABIKI-WAKIJAJUUSTRAIKA wa Brazil, Alexandre Pato, ambae nyota yake imefifia, amekamilisha uhamisho wake kutoka Klabu ya Brazil Corinthians kwenda Chelsea kwa Mkopo wa Miezi 6.

Chelsea imeshaafikiana maslahi binafsi na Mbrazil huyo wa Miaka 26 huku lengo likiwa ni kuufanya uhamisho PATOhuo uwe wa kudumu mwishoni mwa Msimu.

Pato, ambae ameichezea Brazil mara 27 na kufunga Bao 10, hajaitwa kwenye Kikosi hicho tangu 2013.

ANDROS TOWNSEND: ATUA NEWCASTLE TOKA TOTTENHAM!
Newcastle wameafikiana Dau la Pauni Milioni 12 na Tottenham ili kumsaini Winga wa England Andros Townsend.
Townsend, mwenye Miaka 24, Msimu huu ameichezea Tottenham mara 3 tu kwenye Ligi Kuu England na mara zote alitokea Benchi.

Townsend anaungana na Wachezaji wapya Jonjo Shelvey na Henri Saivet ambao Newcastle wamewasaini kwenye Dirisha la Uhamisho la hii Januari.
Townsend alianzia Soka lake kwenye Chuo cha Soka cha Tottenham tangu akiwa na Miaka 8 na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza ya Klabu hiyo kwenye Msimu wa 2013/14.

Lakini hivi karibuni amekuwa na bifu na Meneja Mauricio Pochettino baada ya kugombani na Mkufunzi wa Viungo wa Timu hiyo, Nathan Gardiner.
WAKATI HUO HUO, Tottenham itamkosa Beki wao Jan Vertonghen kwa Miezi Miwili baada ya kuumia vibaya Goti Jumamosi walipoifunga Crystal Palave 3-1.

Vertonghen, Mchezaji wa Kimataifa wa Belgium mwenye Miaka 28, alitua vibaya baada ya kupigwa kipepsi na Mchezaji wa Palace Connor Wickham ambae Chama cha Spka England, FA, kimemfungulia Mashitaka kwa kosa hilo.

MAN UNITED, VAN GAAL WAREJEA MAZOEZINI!
Manchester United Leo imerejea tena Mazoezini chini ya Meneja wao Louis van Gaal ambae anasakamwa na kuvumishwa kufukuzwa baada ya Jumamosi kufungwa 1-0 na Southampton Uwanjani Old Trafford.

Kipigo hicho ni cha 6 kwenye Ligi Kuu England Msimu huu na kimewaacha Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 Tottenham na Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City.

Mara baada ya Mechi hiyo kwisha Mashabiki Uwanjani Old Trafford walimzomea Van Gaal na kumtaka aondoke Klabuni hapo.

Huku Van Gaal akiripotiwa kwenda kwao Netherlands na Timu kufutiwa Mazoezi ya Siku mbili, Jumapili na Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ed Woodward, alifanya mazungumzo na Wachezaji waandamizi wa Klabu hiyo kutaka kujua kulikoni.

Mechi inayofuata kwa Man United ni Ijumaa Ugenini na Derby County kwenye Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP.

Ikiwa Man United watatupwa nje kwenye Kombe hilo ambalo hawajalichukua kwa Miaka 12 sasa, basi Van Gaal atakuwa tena kwenye lindi la presha ya kutakiwa afukuzwe.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply