Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba
SC, kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo miaka ya
1998-2000 Seleman Said ‘Yeltisn’ kilichotokea jana jijini Dar es
Salaam.
Katika
salamu hizo TFF imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, ambaye
alingoza klabu ya Simba SC na kupelekea kupewa jina la utani la
‘Yelstin” kutokana na ufanisi wake katika kazi na misimamo akifananishwa
na aliyekua Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris Yeltsin.
TFF
kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya
Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa
klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi
hiki cha maombelezo.
Mazishi ya marehemu Selaman Said ‘Yelstin’ yalifanyika leo saa 10 kamili jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni :