SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / WENGER ATOBOA OZIL, SANCHEZ FITI KUIVAA CHELSEA JUMAPILI.

ARSENAL-OZIL-SANCHEZArsene Wenger amedokeza kuwepo wa Mastaa wake wakubwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Jumapili Uwanjani Emirates dhidi ya Mahasimu wao wa Jiji la London Chelsea.

Mechi hii ni muhimu mno kwa Arsenal kushinda na kuuendelea kuongoza Ligi lakini wanakutana na Chelsea ambayo hawajaifunga tangu 2011.

Hivyo kuwepo kwa Ozil na Sanchez ni kitu muhimu kwa kujiimarisha kwao kufuatia Sare mbili mfululizo katika Mechi zao zilizopita za Ligi dhidi ya Liverpool na Stoke City. 

Wakati Ozil ameikosa Mechi tu, ile na Stoke City, akiwa na maumivu ya Nyonga, Sanchez hajacheza tangu mwishoni mwa Novemba akikabiliwa na maumivu ya Musuli za Pajani.

Lakini Wenger ana matumaini makubwa kuhusu Mastaa hao wawili na ameeleza: “Habari njema ni kuwa Ozil atakuwepo na kwa Sanchez, Siku 2 zijazo ni muhimu, lakini nadhani atakuwepo kwenye Kikosi ili tuchague Timu.”

Kuhusu Majeruhi wao wengine, Wenger amesema Francis Coquelin amerejea Mazoezini hii Leo wakati Danny Welbeck ataanza Mazoezi Wiki ijayo na Tomas Rosicky tayari yupo fiti na anatarajiwa kucheza Mechi ya Vijana wa Chini ya Miaka 21 Ijumaa Usiku.

LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo            
Jumamosi 23 Januari 2016
1545 Norwich v Liverpool           
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Crystal Palace v Tottenham         
Leicester v Stoke             
Man United v Southampton                  
Sunderland v Bournemouth                  
Watford v Newcastle                  
West Brom v Aston Villa             
2030 West Ham v Man City         
Jumapili 24 Januari 2016
1630 Everton v Swansea            
1900 Arsenal v Chelsea

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply