Mambo
yakikaa sawa basi baada ya miezi michache mno, Simba itakuwa na uwanja
wake bomba wa mazoezi wenye kiwango kizuri kwa ajili ya kujifua na
michuano mbalimbali.
Iko
hivyo kwa kuwa wiki iliyopita tayari uongozi wa Simba umefanya
mawasiliano na moja ya kampuni za nchini China na kuwapa oda ya
kuwatengenezea nyasi bandia ‘kapeti’ kwa ajili ya uwanja wao uliopo
Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar.
Tayari
kila kitu kimekamilika na kampuni hiyo imewaeleza kwamba takriban baada
ya wiki tatu kila kitu kitakuwa tayari na mzigo utatumwa mapema mno.
Wakati
hayo yakiendelea juzi Jumamosi, Rais wa Simba, Evans Aveva na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe,
walikwenda kutembelea kiwanja hicho kuangalia kinachoendelea baada ya
kuamuru kufanyika kwa matengenezo ya awali kwa kuuweka sawa udongo huo
wa uwanjani hapo kisha mengine yafuate.
“Tumeshaagiza
hizo nyasi na kila kitu kinakwenda sawa, kwa kuanzia ni kutafuta
‘pitch’ ya kuchezea kwanza kisha mengine kama uzio yatafuata. Baada ya
kufika kwa nyasi, utengenezwaji na uwekwaji wa nyasi hizo huchukua kama
siku sita mpaka 10.
“Kwa
hiyo kwa mahesabu hayo unaweza kuona inaweza kuchukua kama mwezi na
nusu hivi na tunayoyapanga yakakaa kama tunavyotaka,” alisema Hans
Poppe.
Hakuna maoni :