SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KIIZA APIGA BAO MBILI NA KUMPITA AMISSI TAMBWE WANAYEKIMBIZANA NAYE.


Sasa imekuwa ni toka nikae, toka nikae. Kwani mshambuliaji Hamisi Kiiza wa Simba, leo amekaa kileleni katika ufungaji bora.

Kiiza amefunga mabao mawili wakati Simba ikiiangusha Ndanda FC kwa mabao 3-0, sasa amefikisha mabao 18 huku Tambwe akiwa na mabao 17.

Tambwe alifikisha 17 jana baada ya Yanga kuitwanga African Sports kwa mabao 5-0 huku yeye akifunga mawili na kumpita Kiiza aliyekuwa na 16 wakati yeye alikuwa na 15.

Kiiza raia wa Uganda na Tambwe kutoka Burundi wamekuwa wakichuana kwa kasi kubwa katika ufungaji wa mabao.


Wakati ligi inaendelea, hadi sasa hakuna uhakika kati ya hao wawili nani anaweza kuwa mfungaji bora msimu huu au kuna mwingine ataibuka na kuwapita.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply