SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MAGUFULI Tupatie Mashamba Tukalime Baba, Juzi Umeagiza Tukamatwe, Tupelekwe Kambini Tulime Kwa Lazima.

MAGUFULI tupatie mashamba tukalime baba, jana umeagiza tukamatwe, tupelekwe kambini tulime kwa lazima.

Hakuna haja ya kukamatwa baba, tupatie tu mashamba tutalima wenyewe, kule vijijini kila pori tunalogusa tunaambiwa la ‪#‎MWEKEZAJI‬, kila shamba tunaloliona tunaambiwa la ‪#‎MHESHIMIWAFULANI‬.

Hakuna mashamba ya wazi baba, hata serikali imegawa mashamba yake kwa ‪#‎WADOSI‬.
Tusaidie pia na vitendea kazi, hata majembe ya ‪#‎NGWAMBA‬ tu baba. Mbolea Na umwagiliaji tutamwachia tu ‪#‎MUNGU‬ ataleta neema zake baba.

waangalie na TIB na Benki ya Kilimo baba kama mikopo yao inawafaa vijana unaowakurupusha leo!... Benki zako zinawafaa zaidi wazee kukopa kuliko sisi vijana baba.
Tafadhali sana baba usitufukuze tu bila kujua tutakapoelekea

By Habibu Mchange

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply