SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / UEFA CHAMPIONZ LIGI: KEPTENI JOHN TERRY NJE CHELSEA IKIIVAA PSG JUMATANO.


UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
JUMATANO 9 MAR 2016
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza

2000 Zenit St Petersburg v Benfica [0-1]
2245 Chelsea v Paris St Germaine [1-2]

CHELSEA-TERRYKEPTENI wa Chelsea John Terry ataikosa Mechi muhimu ya marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, dhidi ya Paris St Germaine Uwanjani Stamford Bridge Jumatano Usiku ambayo wanapaswa kupindua kipigo cha 2-1 ili kutinga Robo Fainali.

Terry hajaichezea Chelsea Mechi 5 zilizopita baada ya kuumia kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi uliopita walipoichapa Newcastle 5-1.

Kumkosa Terry ni pengo kwa Chelsea ambao inabidi wamchunge mno Straika hatari wa PSG Zlatan Ibrahimovic ambae anasaka Bao 1 tu kufikia Bao 50 kwenye Mechi za Ulaya na kuwa Mtu wa 14 kutimiza idadi hiyo.

Lakini Chelsea watapata ahueni kidogo kwani Straika wao Diego Costa, ambae aliikosa Sare ya Wikiendi ya 1-1 na Stoke City kutokana na maumivu, sasa yuko fiti kuivaa PSG.

Huu ni Msimu wa 3 mfululizo kwa Chelsea na PSG kukutana kwenye hatua za Mtoano za UCL na kila Msimu Timu moja imefuzu kwa mgongo wa Goli za Ugenini.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Chelsea: Courtois; Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Kenedy; Mikel, Fabregas; Hazard, Oscar, Willian; Diego Costa
Paris Saint-Germain: Trapp; Van Der Wiel, Luiz, Silva, Maxwell; Matuidi, Verratti, Motta; Moura, Ibrahimovic, Di Maria
REFA: Felix Brych (Germany)

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply