Straika
hatari wa Simba, Paul Kiongera, amelazimika kushindwa kufika kwa wakati
uliopangwa katika timu hiyo licha ya kupatiwa tiketi, kufuatia
kuitumikia timu yake ya taifa, Harambee Stars ya Kenya kwenye michuano
ya Chalenji.
Kiongera
alitakiwa kuwasili nchini wiki iliyopita ambapo tayari ameshatumiwa
tiketi kwa ajili ya kutua nchini kujiunga na kikosi hicho.
Chanzo
kutoka Simba kimeeleza kuwa, Kiongera atatua nchini mara tu baada ya
kumalizika kwa michuano ya Chalenji inayofanyika Ethiopia.
“Kiongera
alitakiwa kutua nchini tangu wiki iliyopita kwa ajili ya kujiunga na
kikosi kuendelea na mazoezi ili kuongeza nguvu katika timu hiyo.
“Kilichokuja
kutibua katikati ni michuano ya Chalenji, hivyo kusababisha ratiba yake
ya kuja huku nchini kuvurugika hadi itakapofikia tamati,” kilisema
chanzo hicho.
Hakuna maoni :