SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / BARCELONA V ARSENAL JUMATANO - KUIFUNGA ARSENAL EMIRATES SI TIJA, BARCA WASEMA ‘HAPA KAZI TU.

BARCA-ARSENAL-WENGERvMSNKOCHA wa Barcelona Luis Enrique amesema wao hawabweteki na hawatilii maanani kuwa na faida baada ya kuifunga Arsenal 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Emirates bali wataingia ngangari katika Mechi ya Marudiano Jumatano Usiku huko Nou Camp.

Barca wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajafungwa katika Mechi 37 na wameshinda Mechi zao 8 zilizopita huku wakiwania kutinga Robo Fainali ya UCL kwa mara ya 10 mfululizo.

Katika Mechi ya kwanza huko Emirates, Bao 2 za Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi, ndizo ziliwapa Barca ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Robo Fainali ya UCL.

Mechi zao zilizopita za Wikiendi:
Barcelona 6-0 Getafe (Juan Rodríguez 8 Kajifunga, El Haddadi 19, Neymar 32 51, Messi 40, Arda Turan 57)
-Ushindi huu umezidi kuwachimbia Barca kileleni mwa La Liga.
Arsenal 1-2 Watford (Ighalo 50, Guedioura 63; Welbeck 88)
-Kipigo hiki kiliwatupa Arsenal nje ya FA CUP ambayo wao walikuwa Mabingwa Watetezi kwa Misimu Miwili iliyopita.

VIKOSIN VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona: Ter Stegen; Alves, Mathieu, Mascherano, Alba; Busquets; Rakitić, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar.
Hawatacheza: Rafinha (Goti), Sandro (Musuli), Piqué (Kifungo)
Arsenal: Ospina; Bellerín, Mertesacker, Gabriel, Monreal; Coquelin, Elneny; Campbell, Özil, Sánchez; Giroud.
Hawatacheza: Ramsey (Paja), Čech (Musuli), Cazorla (Kifundo cha Mguu), Oxlade-Chamberlain (Goti), Rosický (Paja), Wilshere (Mguu)
Hatihati: Koscielny (Tatizo la Mguu)

REFA: Sergei Karasev (Russia)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven [0-0]
Man City v Dynamo Kiev [3-1]    
JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]

TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply